SEHEMU O1 : Siri Ya Jina lako by Frank Bwenge

 SEMINA YA NENO LA MUNGU

JINA LA SEMINA: SIRI YA JINA LAKO

SEHEMU 01: UDANGANYIFU AU UKWELI KUHUSU MAJINA YA WATU

Transcripted From : youtube channel @bibliatimes

Jiunge whatsapp group 0627945434

 

Haleluya. Karibu sana kwenye semina mpya. Naitwa Mwalimu Frank Bwenge nakukaribisha.

Hii semina inaitwa siri ya jina lako. Nataka nikuambie tu ukweli kwamba watu wengi ni wahanga wa majina yao wenyewe. Watu wengi aina ya maisha wanayoishi, aina ya matatizo wanayokutana nayo, aina ya vikwazo kwenye maisha yao ni kwa sababu hawaijui siri ya jina lao.

Kwahiyo kwenye hii semina tutaenda kujifunza siri ya jina lako. Jina ni nini? Na sehemu ya kwanza nitakufundisha udanganyifu kuhusu majina ambao umeharibu hatima za wengi

 

Kuna vitu ambavyo vipo mtaani. Kuna vitu ambavyo vipo ambavyo watu wamevizoea na wanaona ni kawaida. Lakini nakuambia ni uhadaifu wa shetani kuhusu majina. So lazima ujue hiki kitu kitakusaidia sana. Sema amen. Kabla hatujaendelea naomba tumshukuru Mungu.

Baba asante kwa ajili ya neema hii. Asante kwa kibali cha semina hii mpya. Malango ya masaa haya ninaliinua jina lako na kulitukuza katika jina la Yesu Kristo mnazareti aliye hai. Nenda pamoja nasi ukatufundishe ukatuelekeze katika jinala Yesu. Ninaomba sasa fahamu za watu wako eh Bwana zikafunguke kabisa na kila hila za adui zizipate nafasi. Amen.

 

Karibu sana sehemu ya kwanza ambayo inaitwa Udanganyifu Kuhusu Majina Kutoka Kwa Shetani. Unaweza ukaandika uhadaifu kuhusu majina. Na kuna vitu ambavyo nitakuelekeza leo ambavyo unapaswa uviandike kama sehemu ya utangulizi yaani sehemu hii ya kwanza. Na hakika Mungu anaenda kukubadili, anaenda kukuelekeza vitu vingi sana.

 

Wengi mpaka hii semina inaisha tutakuja kugundua kwanza kuna aina ya mamlaka tumeyakosa kwa sababu hatukujua siri ya majina. Lakini pia tutakuja kugundua kuna aina ya watoto wetu au kuna aina ya maisha tunaishi kwa sababu kuna siri hatukujua kuhusu majina yetu. Sema amina. Karibu sana.

 

Sasa kitu cha kwanza ambacho unatakiwa ukijue

 

NAMBA MOJA #01

Ni kwamba kila kitu kina jina. Kiwe kiumbe hai, kisiwe kiumbe hai kina jina. Kila kitu kina jina. Kila kitu duniani kina jina

Kama Mungu alikipa kila kitu jina maana yake Jina ni muhimu sana na jina unapewa sawasawa na ulivyo ,ukikosea kupewa jina maana haitakuwa kama ulivyo

 

 NAMBA MBILI #02

Jina sio herufi haleluya jina sio herufi. Kuna watu ambao walichokifanya ni nini? Wakati wanaita majina ya watoto wao wakachukua jina lao. Jina la baba labda jina la baba anaitwa John alafu jina la mama anaitwa Dorcas. Alafu yule mtoto akachukua ile “jo” wakaunganisha na “do” kwa hiyo wakamuita JODO. Haleluya. Wakamuita nini? Jodo.

 

Nataka nikuambie kitu kimoja unaweza kuwa umeunganisha vitu viwili ambavyo huvijui. Yaani nikwambie tu kweli kama hawa wazazi wana vifungo. John ana kifungo, Dorcas ana kifungo.Ulichofanya umeunganisha vifungo viwili, matatizo mawili. Lazima ujue kwamba majina sio herufi tu.

 

Mtu ambaye anadhani majina ni herufi atanishangaa. Sasa shida iko wapi?

Very soon nitakuonyesha kimaandiko kabisa ili uelewe ni nini ambacho tunazungumza hapa ili uelewe. Na kwenye haya maandiko tutaenda kusimamia mstari kwenye hii sehemu ya kwanza. Naomba tusimamie mstari ule wa kitabu cha Mwanzo ili ujue kwamba Mungu anaelewa umuhimu wa majina. Mungu ana utaratibu wa kuwapa majina viumbe hai na visivyo hai. Na yeyote ambaye hafuati ule utaratibu maanake anajikuta kwenye changamoto.

Ukisoma mwanzo ya pili kuanzia mstari wa 19 (Mwanzo 2:10-) inasema Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni na kila ndege wa angani akamletea Adam ili aone atawaitaje kila kiumbe hai jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.

Kama Mungu alifahamu umuhimu wa majina nataka nikuambie lazima wewe pia ndani yako ujue kuna umuhimu wa majina. unaona Mungu anazungumza ili aone atawaitaje maana yake ni nini? Kulikuwa na namna kama angewaita angeona kuna shida angerekebisha.

 So Mungu alisimamia utaratibu mzima wa kuwaita majina wale viumbe. Sema haleluya.

Lazima ujue Mungu yuko very serious na majina. na majina sio herufi. Amen. Nitakufundisha mbele hapo kidogo ili ujue kumbe nyuma ya jina kuna nini. Kitu kingine unapaswa ujue jina sio swaga.

 

Jina sio swaga. Kuna watu walitafuta swaga unaangalia basketball unamsikia tu mchezaji anaitwa TONNYKA na wewe unaenda unachukua TONNYKA jina tu unaona linasound vizuri unaona linaswaga kwa hiyo unataka mtoto wako akiwa anaitwa jina lake liwe na utofauti labda wigos wigos

labda unapenda kusikiliza miziki ya dunia alafu kuna sauti tu ukiisikanga unapenda labda labda templo

(Haya majina nayatengeneza tu rafiki yangu sio kwamba yapo. Okay)

Kwa hiyo unasema na wewe mwanangu nitamuita tempo. Yaani swaga fulani hivi. Kuna mama mmoja alinitafuta alipewa majina mtoto wake alafu yeye akaona haya mbona hayasoundi vizuri akaongezea junior

kwa mfano umeenda kwa kwa mchungaji wako kwa padri amekuombea alafu akakupa jina wewe mwenyewe ulienda kuomba jina umepewa jina alafu unapewa jina unaanza kuliona halina swaga

tayari kuna shida sehemu hilo jina litakuja kumtesa huyo mtoto. Sema amina kama unanielewa. So majina hayatolewi kwa swaga ndugu zangu.

Lakini pia jina sio matamshi mazuri. Eh kuna mtu anataka matamshi mazuri kwamba mwanangu akiitwa aitike virahisi. Yaani sio swala la kuitika kirahisi. Sio swala la matamshi magumu. Eh sio swala hilo. Majina ni zaidi ya hicho kitu.

Nataka nikuambie ukisikiliza hadi mwisho wa hii semina

utagundua alafu utaanza kuponywa utafunguliwa kuna vitu utafunguliwa automatic. Haleluya. Lakini lazima ujue pia kuwa tupo sehemu ya PILI

tumeanza namba moja. Nikakuambia kila kitu kina jina. Kiwe kiumbe hai, kisiwe kiumbe hai. Kwa sababu kama havijapewa utambulisho utavijuaje wewe mwanadamu? Utajuaje hili ni jina, hili ni jini ni ndoo, hii ni kiti? Vyote hivyo vina majina.

Alafu namba mbili nimekuambia nikakwambia jina sio herufi, jina sio swaga, jina sio matamshi mazuri. Lakini pia nataka nikuongezee

 

sehemu hii kwenye namba mbili watu hawaitwi majina kwa kuiga. hii siri hii unaweza ukasema mtumishi ndio watu hawaitwi majina kwa kuiga. Sio kwa sababu bibi yako anaitwa hivi na wewe unachukua jina. Mama YAko anaitwa hivi ni jina hii siri nakuambia kwa sababu hata mimi sikuijua. umenielewa? Eh.

So Roho mtakatifu anavyoachilia hili somo Inabidi uwe mtii. Haita make sense hapa mwanzoni lakini nataka nikuambie nikishaanza kukuonyesha maandiko utakuja uelewe. Maandiko yanafunua kila kitu na utaelewa vizuri mno. Sawa? Eh.

 

So lazima ujue watu hawaitwi majina kwa kuiga. Nikupe ushuhuda wa dada mmoja mama yake akiwa huko ambako alikuwa kuna jina alilisikia. mamake alikuwa mkristo lile jina wala hakutaka kufuatilia lile jina ni la wapi of course lile jina lilikuwa ni la kiislamu

 

ukifuatilia ni moja ya wake wale wa yule  muhammad okay so alivyosikia tu mama mmoja amemuita mtoto wake pale akasema nikija kuzaa mwanangu nitamuita hili jina i'm telling alikuja akamuita lile jina lile jina lilimsumbua sana lilimsumbua

hivi haujawahi kukutana na mtoto anaitwa kwa jina fulani alafu anaanza kulikataa anaanza kulia.

Do you think huwa ni emergency? Ni ajali   hapana huwa sio ajali huwa sio ajali so majina hatuiti kwa kuiga. Okay.

 

NAMBA TATU #03

jina lolote. Jina lolote lina sources mbili. Yaani jina vyanzo viwili. Yaani jina lolote ambalo utaita. Sawa? Eh lina vyanzo viwili. Jina lolote ili liwe jina lazima litoke kwenye ufahamu. Umenielewa? Yaani lazima kuwe na ufahamu fulani. Lazima kuwe na maarifa fulani. Umenielewa?

 

Sasa kuna maarifa ya mbinguni alafu kuna maarifa ya duniani. Jina lolote ambalo limetoka katika maarifa ya mbinguni yaani ni jina linatoka kwa Mungu. Maanake ni Mungu ambaye anaweza kutoa jina. Sawa? Eh umenielewa?

jina lolote ambalo haujafunuliwa na Mungu mwenyewe ni hatari Eh. Sasa Mungu anachofanya nini? Anakupa jina alafu wewe ndio unampa jina mtoto. Hivi unadhani kwa nini ah malaika alikuja moja kwa moja na jina la Yesu? Kwa nini malaika walivyoenda kwa Yohana Mbatizaji walienda na jina la Yohana moja kwa moja?

 

 Kwa sababu Mungu anajua adui anaweza kutumia chansi ya jina kuharibu kazi nzima. So lazima ujue source au vyanzo vya majina ni viwili. Aidha kwa shetani au kwa Mungu. Shetani mara nyingi anatumia miungu. Umenielewa? Eh.

Na hapa lazima uwe makini ili ujue jina limetoka kwa Mungu. Kama yule mtu ambaye anatoa jina ni mtumishi wa Mungu kweli ana uhusiano na Roho Mtakatifu. Ukimuomba jina itabidi aidha atafunuliwa na Roho Mtakatifu pale au achukue kwenye bibilia. Lakini ni vyema sana ukajua kwamba jina lolote lazima litaweza kuwa na msukumo either wa Mungu au wa miungu.

Yaani  hiyo we don't discuss. Kwa mfano kuna watu majina yao walipewa na mizimu. Huwezi ukaenda kumuomba jina bibi yako, mama yako ambaye unajua ana abudu miungu. yeye na waganga yeye na matambiko ni damu kwa damu. nataka nikuambie lile jina atalipata kwa ufahamu wa kuzimu kwa ufahamu wa shetani. Kwa sababu mtu yeyote ambaye anamtumikia shetani moja ya kitu ambacho anakuwa amempa shetani ni nafsi na moja ya kitu ambacho kipo kwenye nafsi ni ufahamu.

 

So direct moja ya sehemu ambayo anakuwa shetani ameishika ni ufahamu. Akiona kuna fursa ya kumkamata mtu kupitia jina maanake analiachilia moja kwa moja. Mungu pia anaheshimu majina. Menielewa watoto wa Mungu?

 Usije ukadharau jina rafiki yangu. Kuna kuna baba mmoja na mke wake walikuwa ni  walimu wa vyuoni. Ah miaka ya nyuma huko ,wakati wanaomba wanaomba wakawa wameona jina John. Umenielewa?

 

unajua baada ya mtoto kujifungua wakaona John mbona wako wengi sana ,

 hapa ndio wazazi wengi wamekamatwa mbona kina John wako wengi sana kumbuka hili jina limetoka kwa Mungu wenyewe wakaongezea walimuongezea jina yaani baadala ya kusema John wakamwiita Jordan

Joe waliongezea Yaani kwenye John wakaongeza swaga ninavyokuambia hizo swaga sasa wakavunja kile Mungu amekisema. Huyo mtoto baada ya muda aliwasumbua alikuwa anaugua ovyo ovyo ovyo ovyo. Ukivunja usipomtii Mungu ukamwita jina mtoto ambalo unajisikia wewe umemtii shetani.

 

jina nimekuambia sio herufi jina lina siri kubwa. Ndio maana hii semina inaitwa siri ya jina. Mimi nitakufundisha hapo mbele utaelewa kila kitu.

 

So namba tatu nimekuambia jina linaweza likawa na chanzo cha Mungu au chanzo cha shetani. Why? Kutokana na ufahamu aidha ufahamu wa Mungu au ufahamu uliokamatwa na shetani.

 

Namba nne #04

 Mungu anaheshimu sana majina. Mungu anaheshimu sana majina. Ukitaka kujua Mungu anaheshimu majina utaona kwenye maandiko anambadili Abram kuwa Ibrahimu.

 

Anambadili Simoni kuwa Petro. Anambadili Sauli kuwa Paulo. Lakini huyu Mungu ukitaka kujua anaheshimu majina anamuita Adam kwenye Mwanzo 2:19- 20 anamwambia wape majina.

Lakini pia ukitaka kujua Mungu anaheshimu majina andika ni kwamba yeye mwenyewe ana jina. Haleluya. Yeye ndiye Mungu. Haleluya.

Na Mungu anaheshimu majina. Kwa sababu gani? Moja ya kitu ambacho Mungu anakiheshimu ni jina lake. Ukitaka kujua Mungu hata  Mungu anavyokupa huduma anakupa huduma kwa ajili ya utukufu wa jina lake.

 

Unajua kipindi cha ufalme wa Hezekia ufalme wa Ashuru walikuja wakamtukana sana Mungu wa Israeli. Alafu unajua HEzekia alienda na nyaraka. Unajua alienda kumshtaki na nini? Alishtaki akisema jina lako wamelitukana.

USICHEZE na jina la Mungu ndio maana moja ya amri NI usilitaje bure jina LA MUNGU. Maana yake nini? Jina la Mungu analiheshimu kuliko kawaida. Ulitajitaji tu. Umenielewa? Sasa sisi tumekuwa wakristo ambao tunaita majina tu ovyo. Unakutana tu na jina flongo na wewe unamuita mtoto frongo. Unakutana na jina huko shopping na wewe shopping.

 

You see

kama Mungu mwenyewe anaheshimu jina lazima ujue. Sisi alituumba kwenye sura na mfano wake. Kile ambacho Mungu anapenda lazima tukipende. Asichokipenda hatupasi kukipenda. anachokiheshimu tunapasa kukiheshimu.

Haleluya.

Ukisoma kutoka 3:14 utagundua Musa anamuuliza Mungu kutoka 3:14 Mungu akamwambia Musa. Musa baada ya kuuliza sasa okay ngoja nikusomee hapa juu kuanzia kutoka 3:13- 14 Musa akamwambia Mungu tazama nitakapofika kwa wana wa Israeli na kuwaambia Mungu wa baba zenu amenituma kwenu nao wakiniuliza jina lake ni nani niwaambie nini?

Ndio maana kila kitu lazima kiwe na jina kwa sababu ndio njia pekee ya utambulisho sema haleluya alafu mstari wa 14 Mungu akamwambia Musa mimi niko ambaye niko akasema ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli, mimi Niko amenituma kwenu.

Haleluya.

Unajua Mungu alikuwa anamaanisha nini? Hana jina moja. Yeye ni Mungu ambaye anajifunua sawasawa na ulivyomuita. Yeye ni Mungu ambaye anajifunua sawasawa na wewe ulivyomuita. Ndio maana ukisoma bibilia utagundua Mungu ana majina mengi na majina yote mazuri ya utukufu ni majiNa ya Mungu mwenyewe. Sema amina.

 

So hii sehemu ya kwanza nataka uelewe hivi vitu vikusaidie na utagundua kwamba Mungu ana majina mengi sana kwenye Bibilia.

 

ukianza na anajulikana kama mimi niko yaani Jehova au Yahwe hilo ndio jina ambalo Mungu anajipa okay kusoma kutoka 3:14

lakini kuna jina jingine anajiita Jehova JiRe. Hii utasoma Mwanzo 22:14. Mwanzo 22:14. Naomba nikusomee haya ni majina ya Mungu. Na muda mwingine angalia shida gani unaipitia. Kwa mfano unahitaji uponyaji anaitwa Jehova RAPHa maanake Mungu anayeponya.

Ukisoma Mwanzo 22:14 inasema Ibrahimu akapaita mahali hapo Jehova jiRe kama watu wasemavyo hata leo katika mlima wa Bwana itapatikana.

Haleluya.

Hii inamaanisha nini? Bwana atatualizia au Bwana atatupatia mahitaji yetu. Okay. Yes. Kasome. Ukisoma stori nzuri ya Ibrahimu alivyokuwa anaenda kutoa nini? Kumtoa sadaka mwanaye. Alafu ghafla Mungu akampatia kondoo. Haleluya.

So alivyokuwa anaenda mtoto wake alimuuliza baba mbona naona kuni naona kila kitu mwanakondoo yuko wapi? Akasema Bwana atatuPATia Bwana atatupatia. Haleluya. Haleluya.

So jina la kwanza ni ya ni Yahwe au Jehova au mimi niko ambao ni kutoka 3:14. Jina la pili ambalo nataka nikufundishe sitakupa majina yote. Okay. Ah sitakupa majina yote. Ni majina mengi sana. Okay.

 

Jina jina jina la pili nimekuambia ni nini? Ni Jehova JIRE. Jina la tatu ni Jehova Nissi Bwana ni bendera yangu. Soma kutoka 17:15. Kutoka 1715.

 

Jina la nne ni Jehova Shalom. Haleluya. Jehova Shalom. Hiyo ni namba nne. Bwana ni amani yangu. Hiyo ndio maana yake. Okay? Soma waamuzi 6:24. Na hii ukisoma utaelewa ilikuwa ni pale ambapo Gideon alipompokea Mungu kama amani yake. Alikuwa mtu ambaye anajificha. Hata kipindi ambacho malaika anamtokea alikuwa amejificha. So Gideon baada ya kuona Mungu amemtokea anamtambua kama Bwana ni amani yangu yaani Jehova Shalom.

Lakini namba tano ni El Shaddai , Mungu mwenye nguvu zote. Soma kitabu cha Mwanzo 17:1 ndivyo ambavyo Mungu alijifunua kwa Ibrahimu. Okay.

namba sita. Elohim yaani Mungu muumba. Ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:1 Bibilia inasema hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Huyu Mungu ukienda kusoma kwenye lugha ya wenzetu ilitolewa kutoka kwenye neno inaitwa Elohim. Yaani Mungu muumba. Elohim.

Namba saba anajulikana kama Jehova Adonai. Yaani Adonai Bwana au mkuu. Hiyo ndio maana ya Adonai. Okay. Na hii inatumika kumaanisha Mungu kama mtawala na Bwana. Haleluya. Haleluya. Haleluya.

 

So majina ya Mungu ni mengi. Jina jingine nikuongezee Jehova TSdikenU. Okay.  Maana yake Bwana ni haki yetu. Hii nikutajie ni T S I D K E N U Haleluya. Haya ni majina ambayo Mungu nataka nikuonyeshe umuhimu wa majina.

Kama Mungu alijifunua katika lazima kwanza ujue Mungu ni tofauti. Jina la Mungu ni tofauti na majina mengine yoyote. Yaani jina la Mungu lenyewe linanyumbulika

kutegemeana na wewe unataka upo kwenye shida gani ndio maana majina mazuri yote ni ya nani? Ya Mungu. Majina yenye utukufu yote ni ya nani? Ni ya Mungu.

 

So najaribu kukupa majina yenye utukufu

Bwana ni haki yetu. Soma yeremia 23:6. Yeremia 23:6  mstari wa sita inasema katika siku zake yake Yuda ataokolewa na Israeli atakaa salama na jina lake atakaloitwa ni hili Bwana ni haki yetu.

Okay. Sasa kiyahudi maana yake nini? Kiyahudi ni Jehova Tsdikenu. Okay. Yes. Yaani Bwana ni haki yetu.

Jina jingine ni Jehova Shamah. Maana yake nini? Bwana yuko hapo. Okay. Ukisoma. Ezekieli 48:35 kuuzunguka ni mianzi 18,000 na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili. Bwana yuko hapa. Bwana yuko hapa inamaanisha Jehova Shama.

 

Lakini pia namba 10 I think namba 10 Jehova rohi. Hii ndio ile ile zaburi ya 23 tunaitanga ni zaburi ya Jehova rohi. Okay. Yote hayo ni majina. So Jehova rohi Bwana ni mchungaji wangu.

Soma Zaburi ya 23:1. So ukitaka Mungu ajifunue kama mchungaji wako maanake unamuita kama Jehova rohi. Jehova rohi. Okay? Lakini kama ukihitaji Mungu ashuke kama mponyaji, yaani Jehova rapha, Bwana anayeponya utamuita kama Jehova rapha. Okay. Kutoka 15:26. Tusome kutoka 15 26 inasema nini?

 

Akawaambia kwamba utaisikiliza oh sorry kutoka 15 kutoka [Muziki] 15 26 yaani yenyewe akawaambia akawaambia kwamba utaisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wako na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake yake na kutega masikio usikie maagizo yake na kuzishika amri zake. Mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri kwa kuwa mimi ndimi Bwana nikuponyaye. Ndio maana kuna nyimbo inaitanga wewe ni bwana uniponya maanake ni Jehova Rapha kutoka 15:26 haleluya

 

kuna Jehova sabaoth bwana wa majeshi bwana wa vita kasome 1 Samueli 1:3

 

kuna Jehova Elyon  maana yake Mungu aliye juu sana kasome mwanzo 14:18

El roi mana yake “Mungu aonaye’ Mwanzo 16:13

Lakini pia Mungu anajifunua kama EL elom yaani Mungu wa milele. Soma Isaya 40:28.

Alafu kuna mahali anajifunua kama Jehova qanna  yaani Mungu mwenye wivu. Kasome kutoka 34:14. Haleluya.

Kuna kitu utakuwa umejifunza hapa kwamba majina pia ni utambulisho majina pia yanazungumzia tabia. Yanasema wewe ni nani. Ukikosea jina mtoto wako ukamuita taabu. Mh. Ndio taabu imekuja. Eh.

Nimekuambia cha kwanza namba moja kila kitu kina jina. Na kama kila kitu kina jina hupaswi kudharau kwa sababu jina kwa alama ya mwanzoni ni utambulisho tutakujua kwa jina lako. Okay?

Lakini pia nikakuambia kwamba jina sio herufi, jina sio swaga, jina sio matamshi mazuri. Watu hawaitwi majina kwa kuiga.

Na namba tatu nikakwambia kutoka hapo juu kwa sababu hatuiti kwa kuiga. maanake jina lolote either linaweza kutoka kwa Mungu au kwa shetani. Hamnanga mtu kati. Okay. Nakumbuka haya majina yote ambaye ataita ni mwanadamu. Maanake Mungu anaweza kutumia mwanadamu. Shetani anaweza kutumia mwanadamu kuita hayo majina. Haina maana shetani atakuja kuita majina yeye mwenyewe.

Namba tatu.

Okay. Namba namba tatu ah ni hiyo.

Namba nne Mungu anaheshimu sana majina. Nikakuonyesha yeye mwenyewe ana majina. Haleluya. Lakini alimuita Adam akamwambia wape majina. Lakini tunaona hata Yesu baada ya kufufuka zawadi aliyopewa ni jina.

Lazima ujue Mungu anaheshimu majina kiasi gani. Haleluya. Ehe. Eh so Mungu ana majina mengi na wewe ndio utaamua ajifunue kwa jina lipi? Ndio maana anakwambia Mungu sio mwanadamu. Umenielewa? Eh yes. Wewe mwanadamu na jina moja lakini Mungu anaweza kujifunua tofauti.

Haleluya. Haleluya. Hii semina itakusaidia vitu vingi. Mi nakuambia wewe endelea kunisikiliza hadi mwisho. Hautabaki hapo ulipo. Okay? Yes.

Hautabaki ulipo hapo.

Mungu wa mbinguni akusaidie sana sana. Lazima ujue kuyatumia haya majina ya Mungu. Kuna wakati un upo kwenye vita maanake utamuita kama nani? Sabaoth bwana wa majeshi. Kuna wakati ndugu yangu umenielewa? Eh. Kuna wakati una magonjwa unapitia shida utamuita kama Jehova Jehova rapha. Umenielewa?

Kuna wakati utaona kama Mungu maeneo kama vile Mungu hayupo. Ni kama vile kuna nguvu zingine. Eh hapo unaweza ukamuita pia kama Jehova Shama. Haleluya.

Hiki kitu kikusaidie wewe kuelewa unapokuwa unaomba. Ndio maana utakuta wenzio wanatamka maneno mengi kwenye maombi kwa sababu sometimes ni maarifa kama haya.

Anamuita Mungu kwenye angle tofauti tofauti tofauti tofauti. Remember unapoita jina huiti herufi. Nimewaambia sio matamshi unayotamka sio sauti ile inayotoka. Yes. Nitakufundisha nyuma ya jina kuna roho. Nitakufundisha. Haleluya

. So unapoliita jina la Mungu sifikiri unaita tu herufi. Hapana. Sema amina.

Yesu anasema maneno niwaambio. Maneno niwaambiayo ni roho. Maana yake jina ni maneno yanayotoka. Nyuma yake yana roho. Haleluya. Sio maneno pekee yake. Ni maneno ambayo nyuma yake yana roho.







Post a Comment

Previous Post Next Post

Popular Items