MAGONJWA SIO MAPENZI YA MUNGU

 


SEHEMU YA PILI

MAGONJWA SIO MAPENZI YA MUNGU

Ukweli ni kuwa bado kuna uongo unatapakaa kwamba kuna watu wanaumwa kwasababu Mungu amewapa magonjwa

Katika agano la kale Mungu alitumia magonjwa kama njia ya kuwaadhibu watu yaani kama laana(Kumbukumbu la Torati 28) kwasababu mauti ilikuwa na nguvu lakini baada ya ufufuo wa Bwana Yesu alivunja laana zote ikiwepo laana ya magonjwa maana ameshinda mauti

Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;’’

Kusema kuwa magonjwa ni mapenzi ya Mungu ni kuitukana kazi ya msalaba maana moja ya sababu ya kwanini Yesu alikuja duniani ilikuwa kuyabeba magonjwa yetu tena kwa mateso makubwa

Aliyeyabeba magonjwa ni namna gani anaweza tena kukurudishia magonjwa wewe ?

Bwana Yesu hawezi kuja duniani kuyabeba magonjwa yetu halafu tena baada ya kufika mbinguni arudishe kile ambacho alikifia msalabani

1 petro 2:24Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

Ni wazi uponyaji ni Sehemu ya mpango wa uponyaji wa MUNGU kwa wanadamu sawasawa na ilivyo maondoleo ya dhambi

Kusema magonjwa ni mapenzi ya Mungu nis awa na kusema kwamba Kutenda dhambi ni mapenzi ya Mungu maana vyote ni Sehemu ya mpango wa ukombozi

Kama ambavyo unaichukia dhambi ndivyo unapaswa pia kuchukia magonjwa maana vyote Mungu alivitazama na kutuma mwanae ili tusitende dhambi tena na wala tusiugue tena

WatU wengI hawana Imani ya kupona kwasababu ya mafundisho ya uongo kwamba magonjwa ni mapenzi ya MUNGU

Kuna ana miaka 10 anaumwa lakini anajipa moyo akidhani kuwa Mungu anamjaribu kumbe ni kifungo cha adui na kwasababu anadhani ni MUNGU kampa huo ugonjwa hivyo basi hawezi kuchukua hatua yoyote ya Imani ili kupokea uponyaji

Magonjwa yaliingia duniani baada ya Adam na Eva kuanguka dhambini

Mungu hakuwa na mpango wa watu waugue ili wamuogope au kuwajaribu

Siku ambayo Adam na Eva walikula tunda waliingiza mauti duniani na hii mauti ilikuwa na magonjwa ndani yake pia na shetani akaanza kuwatesa watu

Ufunuo 1:18 “na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.’’

Lakini baada ya kifo na ufufuko wa Bwana Yesu ile mauti aliishinda na kutupa funguo sisi wana wa Mungu na hivyo tuna mamlaka ya kuangusha magonjwa na magonjwa kutokuwa Sehemu ya maisha yetu

1 Wakorintho15:55-57:  “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.’’

Magonjwa yote yanatoka kwa shetani na MUNGU hawezi kukupa ugonjwa ili kukujaribu

Ikiwa unasoma nakala hii,Mimi Mtumishi wa Mungu Frank Bwenge nataka ujue kuwa shetani ni muongo na ukiamini kwamba huo ugonjwa sio mapenzi ya Mungu na kisha ukajua kuwa IMANI YAKO ITAKUPONYA Basi inuka na uende katika hatima yako

Acha kulalamika tena kwanini Mungu anakutesa Imnuka ukitambua kuwa uliponywa msalabani na kinachohitajika ni kukataa kuwa wewe ni mgonjwa maana Mungu anasema wewe sio mgonjwa bali umepona

Anza kukiri kwamba kupigwa kwake umepona na wala wewe si mgonjwa (ISAYA 53:5)

SHINDA UONGO HUU

·         Eti ukimkosea Mungu anakupa magonjwa  x

·         Eti Mungu akitaka kukuinua kiuchumi anakupa magonjwa  x

·         Eti magonjwa ni njia ya kukajaribu x

Usije kukubali kwamba ugonjwa wowote umetoka kwa Mungu kwasababu yoyote

Na kama magonjwa yote yametoka kwa shetani basi hayana uhalali kuwepo katika mwili wako

Mungu hawezi kutumia dhambi zako kukupa magonjwa bali shetani hutumia dhambi za watu kama mlango wa kuwazuia katika mambo mbalimbali ikiwepo na magonjwa

Yesu na mkoma kuhusu mapenzi ya Mungu

Katika huduma ambazo Yesu alifanya kuna Sehemu nyingi anaonyesha wazi kwamba sio mapenzi ya Mungu watu kuugua na wala Mungu hafurahii watu kuugua

Marko 1:40-42: “Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi akipiga magoti, akamwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. Yesu, akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka; takasika. Mara ukoma ukamtoka, akatakasika.”

Ukisoma hilo andiko juu utagundua kuwa mkoma alianza na swali ili kujua kama ni mapenzi ya Mungu yeye kuponywa na Yesu anamjibu NDIO ni MAPENZI YA MUNGU

Sasa kipindi hiki wakoma walionekana wachafu kiroho na kimwili na walionekana kana kwamba wamefanya dhambi kubwa sana na hivyo walitengwa

Walawi 13:45-46:  "Mwenye ukoma atakuwa na nguo zilizoraruliwa, kichwa chake kitaachwa wazi, atafunika juu ya mdomo wake na kupaza sauti akisema, Najisi! Najisi! Atakaa peke yake, nje ya kambi ndipo atakapokaa.

Japokuwa mkoma huyu alionekana ni mtu asiyefaa lakini tunaona Yesu anamponya

Usijali pengine kuna muda unajihesabia hatia na kuona kama hutapona kwasababu ya aina ya maisha ambayo ulikuwa unaishi lakini kama YESU alivyomponya mkoma hata wewe anaweza kukuponya leo,unapaswa KUAMINI TU

 

Mungu anataka tufanikiwe pia katika afya

Huwezi kuwa Tajiri wa afya ikiwa unateswa na magonjwa na kama Mungu anataka ufanikiwe katika afya yako maana yake si mapenzi yake kukupa wewe ugonjwa

3 Yohana 2:1 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Huruma kama mapenzi ya MUNGU kuponya

Ukifatilia huduma ya Yesu utagundua kuwa alianza na kuwahurumia , ni wazi Aliona namna adui aliwatesa watu hawa na akaugua moyoni mwake

Mathayo 14:14 “Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.’’

Mungu hafurahii kukuona wewe unaumwa na wala usidhani ndio unajisadaka kwake kwa kukubali kuumwa bali unaaibisha kazi ya msalaba na unapaswa kuinuka na kulidhibitisha neno lake kuwa KUPIBWA KWAKE SISI TULIPONA

Yesu anakiri kuwa magonjwa ni kazi ya shetani

Matendo ya mitume 10:38 “habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.’’

Tunaona wazi katika andiko hili kuwa moja ya njia ambayo ibilisi anatumia kuwaonea watu ni magonjwa

Magonjwa ni silaha ya shetani na wala sio Mungu 

Post a Comment

Previous Post Next Post