SEHEMU YA KWANZA
HAKUNA UGONJWA UNAMPATA MTU BILA
KUURUHUSU
Ukweli
ambao watu wengi hawaujui ni kuwa Mungu alivyomuumba mtu ni wazi na Dhahiri
kuwa hakuna chochote kitamuingia bila yeye mwenyewe kusema “NDIO INGIA”
Hakuna
ugonjwa wowote ambao unaweza kukupata kama hujauruhusu kwa kusema “NDIO”
Unaweza
ukakataa kwamba hujawahi kuruhusu ugonjwa ukuingie lakini lazima ujue ulimwengu
wa roho hauongei kwa maneno tu bali kwa HISIA,MATENDOna MAWAZO
Kwasababu
shetani anajua hana mamlaka yoyote kwa mwana wa Mungu na hawezi kukudhuru tu
kama anavyotaka, basi hutanguliza MTEGO kwanza na kwa kushindwa kuutegua
ANAPANDA PANDO lake
Upande
wa magonjwa mtego mkubwa bi dalili za mwanzo na hu oni mtego na namna unapokea
hiyo taarifa itaamua kunaswa kwako au kushindwa kwa adui
Mithali 6:2 “Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno
ya kinywa chako,’’
NAMNA
TUNARUHUSU MAGONJWA KUINGIA
Kuna
njia nyingi ambazo huwa zinatafsiri kwamba tumeruhusu ugonjwa kuingia ndani ya
miili yetu
a. Mawazo
Pale
unapohisi dalili yoyote katika mwili wako halafu katika Mawazo ukajiona namna
umelazwa au namna unateswa na ule ugonjwa ni tafsiri ya kuruhusu ugonjwa uingie
ndani yako
Adui
siku zote hutumia dalili na Mawazo yako yakiruhusu dalili hizo basi umeruhusu
ugonjwa ,ni vyema kutambua kuwa kama mkristo magonjwa yote aliyachukua Bwana
Yesu msalabani na hivyo hayana nafasi kwako
Mathayo 8:17 “ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.’’
Pale
unapohisi dalili za ugonjwa Fulani haijalishi umeumwa mara ngapi usikubali
Mawazo yako kuona tayari ni mgonjwa maana huko ni kuuruhusu ugonjwa
Yesu
anasema kumtamani moyoni mwanamke ni kuzini nae na ndivyo ilivyo unapojiona
tayari mgonjwa kabla ya kuugua ni kuugua
Chochote
ambacho utakiri na kuamini hicho ndicho kinakuwa
b. Hisia
Unapokea
vipi taarifa ya dalili za ugonjwa Fulani ?
Ukweli
ni kuwa namna unapokea taarifa huamua pia kama utaipa nafasi hiyo taarifa au
kuikataa isikudhuru
Imagine
,umekaa tu ndani ghafla ukahisi tumbo linauma halafu taarifa hii ukaipokea kwa hofu
na kukimbilia kunywa Panadol
Hii
inatafsiri tayari umefungua mlango wa tatizo la tumbo kwa njia ya hofu
Ukipokea
taarifa mbaya katika mwili wako usiikubali na wala usiogope tumia neno la Mungu
kama upanga wa Roho kusambaratisha taarifa hiyo
Isaya 53:5” Bali alijeruhiwa kwa makosa
yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na
kwa kupigwa kwake sisi tumepona.’’
Ikiwa
Yesu alipigwa sana na katika kupigwa nilipona na sio nitapona hii ina maanisha
hakuna ugonjwa wenye nguvu juu ya mwili wangu labda kama mimi nitaruhusu huo
ugonjwan
Hivi
unajua kwanini wagonjwa wa UKIMWI huwa wanakufa baada ya kupima na kujulikana
wana UKIMWI?
Hii
ni kwasababu ya hofu inapoingia na kuanza kuwaza namna Maisha yao ni mafupi
Hofu
na Mawazo ni silaha inayoupa ugonjwa nguvu na kumdhuru mwanadamu
Hofu
ni hatari zaidi ya UKIMWI mwenyewe na hakuna ushindi wowote katika hofu
Hofu
sikuzote humtoa Mungu na kumfanya kana kwamba hana msaada kwenye maisha ya mtu
na hapa ndipo shetani hupata nguvu katika ugonjwa au jambo lolote
Shetani
hana nguvu kwa mwanadamu ambayo anatawala Mawazo yake na hana hofu sawasawa na
neno la Mungu
Wagonjwa
wengi wa UKIMWI walianza kukonda na hata kufa baada ya hofu kuingia kwamba wana
UKIMWI japo kabla ya hapo wala hawakuwa na tatizo lolote
Ukweli
mbaya ni kuwa jamii imeaminishwa kwamba UKIMWI unaua ,kwahiyo kila anayepokea
taarifa ana UKIMWI anawaza kufa lakini Mungu wetu anasema kuwa kwa kupigwa
kwake Yesu ,UKIMWI umepona (1 petro 2:24)
Lazima ufike mahali ujue kuwa sisi kama wana
wa Mungu hatusikilizi nini dunia inasema bali mbingu inasema nini na ili ujue
mbingu inasema nini ,soma neno la Mungu
Tambua jambo hili
Namna unapokea taarifa yoyote inaamua kama
utaruhusu tatizo husika au kulikataa
c.
Uovu
Hii ndio sababu pia inayompa nafasi shetani
kupanda magonjwa kwa watu wengi
Mungu hawezi kukupa ugonjwa kama adhabu
lakini shetani anaweza kutumia uovu wako kupata uhalali wa kukupandikizia
magonjwa
Hii ina maanisha kuwa Mungu atakuponya bila
kuangalia uovu wako bali Imani yako na ndio maana Yesu aliponya watu kabla hata
ya kuokoka
Yesu anadhibitisha kwamba ugonjwa ni mlango
wa shetani kupandikiza magonjwa kwa mtu na sio Mungu kumpa ugonjwa mtu
Yohana 5:14 “Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia,
Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo
baya zaidi.’’
d.
Maneno unayojitamkia ndani yako
Hii njia adui huwa anaitumia sana kwa watu
ambao wameponywa tayari
Na hapa pia huwa anatumia dalili zilezile
namna ugonjwa ulianza ,na hii inaweza kuwa maumivu au hali yoyote
Kumbuka zile dalili ni mtego wa wewe ufanye
jambo ndipo ugonjwa uingie
Ukweli ni kwamba watu wengi ambao walipona
halafu wakaugua tatizo lile lile walifanya makosa yale yale ya kuupa nafasi
ugonjwa kwa maneno yao
Kitendo cha kuhisi dalili za ugonjwa wa
kwanza na kukubali kwa maneno kama vile “kumbe sikupona’’ au “nimeanza
tena kuumwa’’ hii ni ruhusu unatoa ya huo ugonjwa kurudi
Dalili za ugonjwa sio ugonjwa na lazima
utamke neno la Bwana na sio kuangalia historia ya kwamba hata mwanzo ulipona
ukaugua tena
Watu wengi ambao wanapona na kuugua tena ni
kwasababu wameshindwa kushinda maneno ya kujitamkia
Adui anachofanya anakutega kwa dalili Fulani
na ukikubali tu anakunasa
Mithali 6:2 “Basi umetegwa kwa
maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,’’
USHUHUDA WA DADA
Kuna dada mmoja niliwahi kumuombea na Bwana
akamponya , na kabla sijakutana nae alikuwa anaishi TABORA na kipindi nakutana
nae alikuwa amehama tabora
Yeye alikuwa na presha kipindi hicho na ambao
walimchezea ni rafiki zake wa kule Tabora na baada ya kuwa amefunguliwa wakawa
wanatafuta njia ya kupandikiza tena ule ugonjwa
Walichofanya walimpigia simu halafu wakampa
Taarifa ya kifo ya Jirani mwingine ambaye alikuwa anampenda sana japo alikuwa
ameshakufa siku nyingi na akaumia kwanini hakupewa taarifa na wakati moyo wake
unamuuma ndio muda ambao adui alipanda zile dalili za presha na yeye ndani yake
akasema “kumbe sikupona’’ na hapohapo ile presha ikarudi
Hivi unadhani kwanini wachawi au waganga ni
lazima wakutishie watakuua kabla hawajakuua?
Hii ni kwasababu wameshindwa kuua kwahiyo
wanachofanya wanakupa taarifa ambayo itapanda hofu ili wapate mlango kwa wewe
kuanza kuwaza namna unakufa
Shetani sikuzote anatumia taarifa na vitisho
kama silaha ya kumfanya mwanadamu aogope au ajiwazie mabaya kama mlango wa
kumteketeza
Shetani hawezi
kufanya chochote kama wewe mwanadamu hujamruhusu
ZINGATIA HILI
Hakuna jema au baya ambalo litampata
mwanadamu kama hajaamini
Marko 9:23 “Yesu akamwambia,
Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.’’
Neno “yote” ina maanisha ya kutoka kwa
shetani na ya kutoka kwa Mungu
IMANI yako ni mlango wa kupokea mazuri au
mabaya na Imani ni kitu cha kiroho na inaanzia katika kile unakifahamu (Warumi
10:17) - Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la
Kristo.
Mungu atakuonyesha upo katika jumba kubwa
katika ndoto na ili liwezekane hilo atasubiri UAMINI bila kukata tamaa lakini
shetani atakuletea dalili za maumivu kwenye tumbo na ukiona kansa na kuamini
kansa utapokea KANSA
Huwezi kupokea chochote bila kuamini kiwe
kizuri au kibaya
Chagua kimoja kuamini neno la Mungu au
kuamini hisia na kile unachokiona au shetani analeta,maana hata ndoto ni lazima
iwe sawasawa na neno la Mungu ili kuiamini
Umejifunza nini katika Sehemu hii ya kwanza unaweza kutuma
ushuhuda wako kupitia whatsapp 0627945434

