Day 03: Maombi na kufunga siku 7 kavu|| Frank Bwenge

 


*DAY 03: MAOMBI NA KUFUNGA SIKU SABA KAVU*

✝️✝️✝️✝️✝️✝️

*Isaya 58:6-7*

Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?

✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️

Kila tunapofunga Mungu anaachilia neema na nguvu ya kutoka katika mateso

Tunafunga Ili kusaidia wengine pale ambacho tumejinyima katika mwili na roho

*MAOMBI YA LEO*

Baba katika Jina la Yesu,Ninatubu dhambi zangu zote, UOVU na makosa yote

Nitakase Kwa damu Yako takatifu Ee Bwana ,unioshe kabisa niwe safi kama theluji mimi na ukoo wangu wote

Nakataa kila nira ya shetani kwenye maisha yangu,Naikata Kwa upanga wa Roho mtakatifu, ninavaa nira ya Bwana Yesu kuanzia leo Kwa Jina la Yesu

Kifungo chochote kwenye maisha yangu na familia yangu,Toka Kwa Jina la Yesu , Toka usirudi tena ,katika kila kamba kwenye ndoa, uchumi,huduma,uzao,elimu na kila mahali Kwa Jina la Yesu

Tabia zozote mbaya leo nazikataa,sitaki tena ,nataka kuwa kama Wewe Yesu nivute kwako maana niko tayari kutumika kwa Jina la Yesu

Majina na mapepo mliozuia chochote Kwenye maisha yangu TOKAAA LEOOO ,TOKA ACHIA UFAHAMU,TOKA ACHIAA NDOA,TOKAA ACHIA IMANI YANGU,TOKA ACHIA MOYO WANGU ,KWA JINA LA YESU

Najifunika na damu ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu katika Jina la Yesu

KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA ROHO MTAKATIFU

AMINA

Post a Comment

Previous Post Next Post