Day 03: Kuomba kiu ya kutafakari neno la Mungu

 *MADHABAHU YA BIBLIATIMES*


✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️


MAOMBI NA MFUNGO


✝️✝️✝️✝️✝️✝️


*DAY 03:* KUOMBA KIU YA KUTAFAKARI NENO LA MUNGU 


*NENO :* Zab 27:4 SUV

Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na *kutafakari hekaluni mwake*


Moja ya Siri kubwa ambayo Mungu anatufundisha kupitia Mfalme Daud ni nguvu ya kutafakari mazuri Ya Bwana kupitia neno la Mungu 


Ukisoma kitabu cha yoshua utagundua kuwa KUTAFAKARI /MEDITATION ni mlango wa mafanikio kwasababu KUTAFAKARI NDIO NJIA KUU YA KUWA NA IMANI NA KUPITIA IMANI YOTE YANAWEZEKANA


Ni lazima tumuombee Mungu kiu ya KUTAFAKARI ili tuwe na Imani na kupokea uponyaji na yale yote ambao tunahitaji kutoka kwa Mungu 


Njia rahisi ya shetani kukuzuia usipokee Kwa Mungu ni KUHARIBU Imani yako kupitia magonjwa na matatizo mengine ili uone Mungu kakuacha na usimuamini 


*MAOMBI*


1. Baba Ahsante kwa upendo na neema zako ninaomba toba na msamaha unioshe na kunitakasa 

2. Ninaomba kiu ya kusoma na kutafakari neno lako kila mara Bwana 

3. Nguvu yoyote ya adui inayonizuia kwenye ufahamu Toka Kwa Jina la Yesu x5

4. Kila roho za giza zilizofunga ufahamu wangu Toka Kwa Jina la Yesu x3

5. Nakataa mambo mengi na mivurugano ya kila aina Kwa Jina la Yesu x2

6. Nakataa vifungo na maagano yote Kwa Damu ya Yesu x2


(Ahsante Yesu Kwa kunipa kiu ya KUTAFAKARI neno lako)


Mwl Frank Bwenge 

0627945434






Post a Comment

Previous Post Next Post