*MADHABAHU YA BIBLIATIMES*
✝️✝️👇👇👇👇
MAOMBI NA MFUNGO
*DAY 4*: KUKATAA KILA HALI MBAYA YA UCHUMI KWA IMANI
*NENO*: Waebrania 11:1
[1]Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Tunaamini tunahela sio kwasababu tunazo mkono ila kwasababu neno la Mungu linatuita MATAJIRI na kweli ni MATAJIRI maana YESU ALIFANYA MASIKINI NA SISI SASA NI MATAJIRI
kazi iloyopo ni kuhamisha utajiri kutoka rohoni kuja mwilini Kwa kutafakari neno la Mungu kupitia maombi haya mafupi
Waefeso1:3
*Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo*
Sisi tuna baraka zote lkn zipo rohoni tunazihamisha Kwa IMANI yaani Kwa kuamini tunazo hata kama HAZIONEKANI KTK MWILI na hii ndio tafsiri ya ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo
*MAOMBI*
1. Baba Ahsante kwa baraka zote ulizonipa ,Ninaomba rehema pale nilipokataa baraka hizo Kwa kutokuamini x3
2. Nimebarikiwa Kwa baraka zote rohoni na mimi sio MASIKINI kupitia Yesu kristo x3
3. mimi sio masikini Mimi ni tajiri x
Ufunuo 2:9
*Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)*
Mimi si masikini Mimi ni tajiri x2
2 Kor 8:9
*Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake*
(HAKIKISHA katika maombi haya chukua hata nusu saa baada ya kuomba kutafakari maisha Yako na kila mstari ambao nimeandika Ili imani Yako ikae moyoni na sio kichwani ni iwe na matokeo kisha rudia tena hayo maombi kila mara)
Mwl Frank Bwenge
0627945434