Day 05: kukataa kila hali ya magonjwa Ya Imani|| By Frank Bwenge

 *MADHABAHU YA BIBLIATIMES*


✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️


*MFUNGO NA MAOMBI


*DAY 5*: KUKATAA KILA HALI YA MAGONJWA KWA IMANI


*NENO LA MUNGU* ; Matendo ya Mitume 10:38

[38]habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. 


MOJA YA MPANGO WA YESU KUJA DUNIA NI ILI WATU WAPONYWE Kwa maana ya kwamba magonjwa ulikuwa mpango wa shetani 


Lkn biblia inaweka wazi kwamba sisi sio WAGONJWA hata kama tunaona Nje ni WAGONJWA


Isaya 53:5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, *Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona*


BIBLIA HAIKUSEMA SISI TUTAPONA BALI TAYARI TUMEPONA na kwasababu Mungu si muongo hata wewe ambaye unahisi maumivu umepona katika Jina la Yesu inuka tembea 


Yoel 3:10b aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari.


Mungu ni Roho akiponya anaponya roho yako kwanza kuanzia ulimwengu wa roho na ukikiri kwamba umepona Kwa Imani na sio kwasababu husikii maumivu hakika umepona 


Imani huponya watu na imani sio nini unahisi au unaona au unasikia hali gani bali ni KULIISHI NENO likisema umepona wewe hakika umepona hata kama UNAHISI MAUMIVU 



*MAOMBI*


1. NAKUSHUKURU MUNGU ninaomba rehema na unisamehe Yesu 

2. Ninakiri Mimi ni mzima na wala sio mgonjwa tena na napokea Uponyaji wa msalabani NDANI yangu 

3. Kupigwa kwake Mimi nimepona na si mgonjwa tena x 5


(Endelea kukiri kila siki hayo maombi kwenye tatizo ambalo unalo) 


Mwl Frank Bwenge



Post a Comment

Previous Post Next Post