*MADHABAHU YA BIBLIATIMES*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*MAOMBI NA MFUNGO*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*DAY 09:* KUOMBEA IMANI
*NENO LA MUNGU*' 1 Timotheo 4:1
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
Wengi tayari wameshajitenga na imani wamekuwa wasoma nyota ,Waanaabudu vitu kama mafuta,maji,vitambaa,keki n.k
Bahati mbaya hawajui kama wamepotea lakini wanaona kwamba ni sahihi kufanya wanachofanya
Mungu atusaidie sana
Wanapeleka nywele Kwa wachungaji bila kujua ni uganga,Wanapeleka kucha zao kanisani bila kujua ni uganga,wanatembea na mafuta ya upako hawajui kama tayari matumani yao wameweka kwenye mafuta na sio Roho Mtakatifu ndani yao
😭😭😭😭😭😭😭
*MAOMBI*
1. Mungu mtakatifu ninakushukuru Kwa neema ya uzima na kunilinda hata sasa
2. Ninaomba Rehema Bwana na unioshe dhambi zangu kwa damu Yako na hata ukoo wote
3. Ninaomba unitengene na Imani za uongo , Na kama ufahamu wangu umekamatwa Bwana kasema na Mimi katika ndoto au njia yoyote
4. Ninakataa Imani zote za uongo na kuamini katika kristo Yesu pekee
5. Nitenge na kila madhabahu zinazofundisha uongo katika Jina la Yesu
6. Yesu niongezee Imani ,Niongezee imani Bwana
*(Ongeza maombi yako pia )*
Mwl Frank Bwenge
Whatsapp 0627945434