*MADHABAHUYABIBLIATIMES*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*MAOMBI NA MFUNGO WA SIKU 40*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*MWALIMU:* Frank Bwenge
*DAY 10* : KUOMBA NEEMA YA WOKOVU ISIKAUKE
Efe 2:8-10 SUV
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
(*Kama hujaokoka Nitakutumia voice note ili uokoke)*
Tumeokolewa au kupokea wokovu kupitia kazi ya msalaba na matendo mema ni matokeo ya neema hiyo na sio juhudi zetu
Ni vyema kumshukru Mungu na kuendelea kuiombea neema hii Ya wokovu idume kwenye maisha yetu
*MAOMBI*
1. Mtakatifu Mtakatifu ninakushukuru Kwa neema hii ya wokovu niliyopokea bure
2. Popote pale nilipoona kwamba nimepokea kwasababu nastahili ninaomba Rehema zako
3. Ninaomba neema hii ikadumu sikuzote kwenye maisha yangu Ee Bwana.
4. Ninawaombea watu wote Baba wapokee Neema hii ya wokovu Yaani WAOKOKE Ili kuwa sehemu ya ufalme wako
(Ongeza maombi pengine unatamani mmeo au mke aokoke au familia Mungu atafanya)
Mwl Frank Bwenge
0627945434