*MADHABAHU YA BIBLIATIMES*
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*MAOMBI NA MFUNG0
✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
*DAY 11:* KUOMBEA MLANGO WA UCHUMI
*NENO LA MUNGU* : Isa 60:11
Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.
Katika ulimwengu wa roho mlango wa uchumi unaweza kufungwa na hapa hata ufanye vipi kazi huwezi kufanikiwa
Leo tutaombea lango la uchumi Kwa mwaka wote 2025
Ili watu walete utajiri kwako wa kila aina na zile baraka za MUNGU ziweze kukifikia
*MAOMBI*
1. Baba katika Jina la Yesu ninakushukuru na ninatubu dhambi zangu zote
2. Ninaamuru kila mlango wa uchumi wangu iwe wazi kwa jina la Yesu x2
3. Natakasa mikono yangu Kwa damu ya Yesu na kila nguvu za giza nazing'oa Kwa Damu ya Yesu x2
4. Najitenga na kila roho ya umasikini na chuma ulete Kwa damu ya Yesu x2
5. Kila roho za giza zinazofatilia maisha yangu ziniachie Kwa Jina la Yesu x3
6. Navunja kila maagano ya umasikini Kwa Jina la Yesu x2
7. Kila mlinzi aliyekaa kwenye mlango wa uchumi wangu kuzuia fedha na watu sahihi nawapiga Kwa upanda wa Roho,nawateketeza Kwa damu ya Yesu
(ONGEZA maombi Yako pia ).
*Atukuzwe Baba............*